KPA yatikisa tena kwa kuilemea Don bosco TZ

KPA yatikisa tena kwa kuilemea Don bosco TZ

Na CHARLES ONGADI

TIMU ya Vikapu ya akina dada KPA iliendelea kutifua vumbi katika Mashindano ya FIBA Africa Zone 5 baada ya kuishinda Don Bosco kwa alama 70-21 jijini Dar es Salaam, Tanzania, jumamosi.

Ushindi huo unaiweka KPA katika nafasi nzuri ya kutinga katika hatua ya fainali ya mashindano haya.KPA ya Kocha Anthony ‘ Odimwengu’ Ojukwu ilitarajiwa kuteremka uwanjani jana ( jumapili) kuchuana na Reg ya Rwanda katika michuano ambao KPA inapigiwa upatu kuvuna ushindi.

Katika pambano dhidi ya Don Bosco, nahodha Velma Achieng, Rita Onyango, Brenda Wasuda na Betty Kalanga wakicheza kufa na kupona licha ya upinzani mkali kutoka kwà Rehema Silombi, Fatima Idadi na Taudensia Aluoch.Mara ya mwisho KPA kushinda taji hili ni mwaka wa 2017 katika mashindano yaliyoandaliwa jijini Kampala nchini Tanzania.

Hata hivyo, kocha Ojukwu amesema ana wingi wa matumaini kikosi chake kitatamba katika mashindano ya mwaka huu.

You can share this post!

BAHARI YA MAPENZI: Ukatili wa kijinsia ni suala la kimamlaka

Wakazi wa Thika kunufaika pakubwa ukarabati wa barabara ya...

T L