KPA yavizia Equity na kuponyoka na ‘mali’

KPA yavizia Equity na kuponyoka na ‘mali’

Na CHARLES ONGADI

TIMU ya Vikapu ya akina dada ya KPA iliikomoa Equity kwa alama 71-35 katika mechi za Fiba Africa Zone 5 katika ukumbi wa Indoor Stadium, jijini Dar es Salaam, Tanzania, Jumanne.

Ni pambano iliyohusisha timu mbili kutoka humu nchini ambazo zimekuwa zikitambiana kwa kipindi kirefu.Hata hivyo, akina dada wa KPA walionekana kunoa barabara kucha zao kwà pambano hili iliyohudhuriwa na mashabiki wengi.

KPA ilianza makeke yake kwa kuvuna ushindi katika robo ya kwànza kwa alama19-17 kisha wakazidisha makali katika kwa kuibuka na ushindi mwingine wa alama16-10.Wachezaji wa Equity wakiongozwa na Diana Ayodi, J Akinyi na M Otieno walionekana kupunguzwa presha na kuwapatia wapinzani wao akina Rebecca Nkatha, Natalie Mwangale na Velma Achieng’ kutamba.

KPA ilivuna ushindi katika robo ya tatu kwà alama 12-2 kisha kufunga Kazi katika robo ya nne kwà alama 24-6.Baada ya ushindi huo, kocha wa KPA Anthony ‘ Odimwengu ‘ Ojukwu aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa ghera na hatimaye kuvuna ushindi huo mkubwa.

You can share this post!

Kinda wa Gor Mchezaji Bora Oktoba

KINYUA BIN KING’ORI: Matamshi ya Ruto kwa hakika...

F M