Habari Mseto

KQ kuwarejesha nchini Wakenya 167 walioko India

August 13th, 2020 1 min read

AGGREY MUTAMBO na FAUSTINE NGILA

Kampuni ya ndege ya Kenya Airways ina mpango wa kuwaleta Wakenya 167 waliokwama India kwa sababu ya janga la corona.

Habari hizo zilitokea baada ya serikali ya Kenya kuwaagiza Wakenya waliokwama Lebanon kuchukua stakabathi zao kutoka Beirut.

Kamishna wa Kenya nchini India Willy Bett aliambia Taifa Leo kwamba wengi wa watu waliokwama India ni wale walioendea matibabu ama wale wanawalinda wagonjwa huku wengine wakiwa masomoni ama kwa utalii. Watarudishwa Kenya kwa nauli yao.

Ndege yenye usajili KQ 203 inatarajiwa kiuondoka nchini Agosti 19. “Itafika nchini saa tatu kasorobo na nauli itakuwa dola za marekani 950 kwa wasafiri wa ardhi na 675 kwa wasafiri wa kawaida,” Bw Bett alisema.

Kwenye nchi ya Lebanon ambapo mlipuko uliua watu 135 na kujehuri mamia ya watu huku maelfu ya watu yakibaki bila maka0

Serikali ya Kenya ilisema kwamba Wakenya watau waliumia kwenye ajali hio.

Bi Halima Mohamud balozi wa Kenya Kuwait aliambia Taifa Leo kwamba wote walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani wale ambao makao yao yaliharibiwa walipewa mahali pa kuishi,”alisema.