KRA kupiga mnada mizigo iliyoachwa

KRA kupiga mnada mizigo iliyoachwa

Na ANTHONY KITIMO

MAMLAKA ya Ukusanyaji Ushuru ya Kenya (KRA) imepanga kupiga mnada mizigo ambayo imechelewa kuchukuliwa katika Bandari ya Mombasa kuanzia leo Jumatano.

Mizigo hiyo inajumuisha vifaa vya kielektroniki, magari, vyombo vya nyumbani miongoni mwa mingine ambayo imekaa bandarini kwa muda mrefu kupita kiasi.

Mratibu wa KRA anayesimamia maeneo ya kusini mwa nchi, Bw Joseph Tonui, alithibitisha kuwa baadhi ya mizigo itakayopigwa mnada ilikuwa imenuiwa kusafirishwa hadi nchi nyingine za nje.

You can share this post!

Uhuru asifia mchango wa jeshi kuinua uchumi

Joho ashinikiza sera za mizigo bandarini zibadilishwe

T L