Habari Mseto

KRA yashauriwa kuwapa wawekezaji motisha

February 26th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Shirika la Kukusanya Ushuru nchini (KRA) limeshauriwa kuwapa motisha wananchi ili kuimarisha mapato kutokana na ushuru.

Hatua zinazovutia walipaji ushuru nchini zina uwezo wa kukuza tamaa ya kuwekeza katika utengenezaji wa viwanda, na kuimarisha nafasi za kazi.

Hali hiyo inaweza kuisaidia KRA kupata walipaji zaidi wa ushuru, kulingana na Mwenyekiti wa Wahasibu wa Umma Kenya (ICPAK) Julius Mwatu.

Kwa mfano, KRA inaweza kuwapa walipaji ushuru ‘likizo ya ushuru’na kuondoa ushuru unaotozwa mali ghafi inayoagizwa kutoka nje.

Kulingana na mwenyekiti huyo, waajiri pia wanaweza kupewa marupurupu kwa kuwaajiri wafanyikazi waliotoka shule juzi.

Alisema kuna haja ya kuwa na sera zinatia moyo wawekezaji lakini sio zinazowafukuza, kwa lengo la kuimarisha nafasi za kazi nchini.