Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA kuu imepiga breki mamlaka ya ushuru nchini (KRA) kumtimua meneja wa ushuru forodha aliyesimamishwa kazi kutoka kwa makazi yake mtaani Bamburi Mombasa.
Jaji Monicah Mbaru aliagiza KRA isimfukuze Bw Julius Kaiya Kihara kutoka kwa nyumba anamoishi ya mamlaka ya ushuru hadi kesi aliyoshtaki kupinga kutimuliwa kazini kwake isikizwe kuamuliwa.
Jaji Mbaru alisema Kaiya anayewakilishwa na wakili Charles njuru Kihara amethibitisha aliachishwa kazi kwa sababu sisizokubalika kisheria. Kaiya alieleza mahakama aliachishwa kazi Julai 16,2021 baada ya kuhudumia serikali kwa miaka 32 bila kufanya makosa yoyote.
Kaiya alieleza mahakama aliachishwa kazi bila sababu kamili. Kesi itasikizwa Feburuari 19 2022.