KRA yazindua mfumo wa kuunganisha risiti za biashara na mashine zake

KRA yazindua mfumo wa kuunganisha risiti za biashara na mashine zake

NA WANDERI KAMAU

MAMLAKA ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) imezindua mfumo utakaounganisha risiti za biashara na mashine zake za kukusanya ushuru.

Mfumo huo, unaoitwa Tax Invoice Management System (TIMS) unalenga kuweka wazi kiwango cha ushuru inachowatoza wauzaji na wanunuzi.

Mfumo huu ni wa kisasa na unalenga kuboresha uwazi kwenye utoaji wa maelezo kuhusu ushuru kwa umma.

Chini ya mfumo huo, wafanyabiashara watakuwa na nafasi kuthibitisha ikiwa ushuru waliotozwa umeifikia KRA au la.

Utekelezaji wa mfumo huo umekuwa ukiendelea na wafanyabiashara wana siku 34 kununua mashine maalum za kutoa risiti hizo za kisasa.

  • Tags

You can share this post!

Mpasuko Azimio kuhusu ‘mchujo’

Didmus atoweka na umati wa Wangamati

T L