Jinsi ya kuandaa biriani ya nyama ya n’gombe

Jinsi ya kuandaa biriani ya nyama ya n’gombe

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 50

Walaji: 3

Vinavyohitajika

 • nyama kilo 1
 • kitunguu saumu kilichosagwa pamoja na tangawizi kijiko 1
 • pilipili iliyosagwa kijiko 1
 • bizari iliyosagwa kijiko 1
 • mdalasini kijiko 1
 • maziwa mala vijiko 5
 • pilipili mboga 1 iliyokatwakatwa
 • vitunguu maji 3 vilivyokatwa
 • nyanya 8 zilizosagwa
 • nyanya ya mkebe vijiko 4
 • dania
 • viazi 4 vilivyokatwa
 • mafuta ya kupikia
 • chumvi
 • mchele nusu kilo
 • rangi ya manjano na kijani

Maelekezo

Weka nyama kwenye sufuria pamoja na mahitaji yote ya rojo isipokuwa viazi, kitunguu maji, dania na mafuta.

Koroga vizuri, ubandike kwenye meko na uache nyama iendelee kuiva (unaweza ukatumia pressure cooker ili nyama iive haraka na ilainike vizuri).

Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe ya kahawia, kisha kiweke pembeni.

Vikaange viazi kwenye mafuta mpaka viive lakini visiive sana kisha viweke pembeni.

Tazama rojo lako na kama nyama imeiva na limekauka, weka viazi na vitunguu ulivyovikaanga, dania na mafuta na uliache lichemke kwa dakika tano. Rojo lipo tayari.

Endelea na matayarisho ya wali. Unaanza kwa kupika mchele uliooshwa vizuri na ufunike mpaka uanze kuiva kisha mwaga maji.

Urudishe motoni na utie mafuta.

Tengeza shimo upande mmoja utie rangi ya manjano na upande mwingine utie rangi ya kijani.

Funika wali wako uendelee kukauka na kuiva vizuri.

Biriani lipo tayari.

Andaa mezani Kwa kachumbari, pilipili ya kukaanga na ufurahie.

You can share this post!

Dereva chipukizi Yuvraj alenga changamoto mpya kwenye...

Kiunjuri awaonya Ruto na Raila kuhusu wawaniaji

T L