Kimataifa

Kucha na kope bandia zapigwa marufuku bungeni TZ

June 8th, 2020 1 min read

NA MASHIRIKA

Wabunge wanawake wa Bunge la Taifa la Tanzania wamepigwa marufuku na Spika wa bunge hilo Bw Job Ndungai kuingia kwenye majengo ya bunge wakiwa wamevaa kucha na kope bandia.

Bw Ngungai alisema kwamba aliweka amri hiyo baada ya Waziri wa Afya Faustine Ndugulile kuzua hisia kali jinsi kucha bandia zitaweza kuleta madhara mwilini.

Amri hiyo pia itafutwa na wageni watakaotembelea bunge, alisema. Wabunge hao pia walikatazwa kuvaa nguo fupiĀ  kwenye bunge.

Utumizi sana wa kucha hizi unaeza kuleta madhara yafuatayo:

  • Unaweza kuzuia kumea kwa kucha
  • Kemikali zinaztumiwa kuzitengeneza na kuzibandika zina harufu mbaya na ni hatari kwa mwili wa binadamu
  • Kuzitoa huhitaji umakini kama si hivo kunaweza kuleta jeraha kwa kucha za kawaida
  • Utumizi sana wa kucha hizi unaweza kuleta maradhi kwa hivo zinahitaji usafi wa hali ya juu.
  • Kwa watu wenye matatizo ya kiafya zinaweza kuwaletea madhara makuu