Kufa ghafla kwa TB Joshua kwawashtua wafuasi wake

Kufa ghafla kwa TB Joshua kwawashtua wafuasi wake

Na AFP

KIFO cha ghafla cha mhubiri maarufu nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua, almaarufu TB Joshua, kimewashangaza wafuasi wake nchini humo na Afrika kwa ujumla.

Hii ni kwa sababu usimamizi wa huduma anayoiongoza mhubiri huyo haikutoa habari kamili kuhusu chanzo cha kifo chake.

Taarifa ilithibitisha kifo hicho kupitia ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook TB Joshua Ministries jana kwa kusema hivi: “Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua, na kumpeleka nyumbani- kama inavyopaswa kwa mapenzi yake.

‘ Haikuongeza maelezo zaidi.Ilidaiwa kuwa mhubiri huyo aliongea wakati wa mkutano wa washirika wa runinga ya Emmanuel TV Jumamosi jioni na kufariki baadaye.

Mwendazake ni mwasisi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations lenye makao yake makuu jijini Lagos.

TB Joshua ni mmoja wa mhubiri mwenye ushawishi na umaarufu mkubwa kupitia mahubiri yake kwenye runinga na mitandao ya kijamii.

Joshua alijijengea sifa kutokana na tabiri mbalimbali alizotoa na zikatimia, hali iliyochangia wafuasi wake kuziamini.

Hata hivyo, wakosoaji wake hupuuzilia mbali tabiri hizo wakisema zinakanganya na hivyo ni vugumu kuaminika.

Kwa mfano, mnamo Februari 2012 TB Joshua alitabiri kwamba rais wa nchi moja iliyoko kusini mwa Afrika angefariki.

Mnamo Aprili 5 mwaka huo, aliyekuwa Rais wa Malawi Bingu Wa Muthariki alifariki.

Watu wengi walishangazwa na jinsi utabiri wa TB Joshua ulitimia.

Mhubiri huyo pia alidai kutabiri kwamba kungetokea shambulio la kigaidi mnamo Januari 7, 2015 nchini Ufaransa katika makao makuu ya gazeti la kila wiki la Charlie Hebdo.

Watu 12 waliuawa katika shambulio hilo lililotekelezwa na katika makao makuu ya gazeti hilo ambalo huchapisha vibonzo vinavyopendwa na wengi.

Joshua pia ametoa tabiri nyingi ambazo hakuwahi kutimia.

Mojawapo ni utabiri kwamba aliyekuwa mgombeaji urais kwa tiketi ya chama cha Democrat katika uchaguzi wa urais wa 2016 nchini Amerika Hillary Clinton angemshinda Donald Trump wa Republican.

Trump aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.

Mnamo 2014 jengo moja ambalo umiliki wake ulihushwa na Mhubiri huyo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 116. Wengi wa waliofariki walikuwa raia wa Afrika Kusini.

Lakini Joshua alishikilia kuwa kisa hicho kilisababishwa na ndege ya kiajabu iliyoonekana likipaa juu jengo hilo dakika chache baada ya kuporomoka.

Baada ya ajali hiyo mwendesha mashtaka mmoja alipendekeza kuwa kanisa la TB Joshua lishtakiwe.

“Kanisa hilo sharti lichunguzwa na kushtakiwa kwa kutotafuta idhini kutoka kwa asasi husika za serikali kabla kuanza ujenzi wa jengo hilo,” akasema Bw Oyetade Komolafe.

You can share this post!

Pigo kwa Serikali korti ikiruhusu Miguna kurejea

KIVULI CHA BABA YAKE