Kuhimiza mawasiliano ya pande nyingi na kushirikiana kujenga mustakabali mzuri

Kuhimiza mawasiliano ya pande nyingi na kushirikiana kujenga mustakabali mzuri

NA MASHIRIKA

Mkutano wa mwaka 2021 wa Baraza la Asia la Boao umefungwa huko Boao, mkoani Hainan. Katibu mkuu wa baraza hilo Bw Li Baodong amesema, kwenye mkutano huo pande mbalimbali zimepongeza pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwa kuchangia kufufuka kwa uchumi wa dunia, na kutoa sauti ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano ili kulinda utaratibu wa pande nyingi.

Katibu mkuu wa Baraza la Asia la Boao Bw. Li Baodong amesema, kwenye mkutano huo, viongozi na wajumbe kutoka nyanja za siasa, biashara na elimu wamebadilishana maoni, na kuafikiana kuongeza ushirikiano katika kukabiliana na janga la COVID-19, na kuimarisha usimamizi wa mambo ya kimataifa.

Pia wamejadili masuala ya kufufuka kwa uchumi wa dunia, na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na kutaka kuimarisha mawasiliano na ushirikiano ili kulinda utaratibu wa pande nyingi.

Amesema, “Biashara kati ya nchi zilizojiunga na pendekezo la ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ imeongezeka hata wakati ikikabiliwa na athari ya janga la COVID-19. Hivyo pendekezo hilo limekuwa mstari wa uhai unaotegemeka. Pande husika zinaona pendekezo hilo lina uhai mkubwa, na linaweza kuunganishwa na mipango ya maendeleo ya nchi nyingine na mapendekezo mengine ya pande nyingi.”

Huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Asia la Boao. Bw. Li amesema katika miaka hiyo iliyopita, baraza hilo limetoa mchango muhimu kwenye kukusanya maoni ya pamoja ya Asia, kuhimiza maendeleo ya bara hilo, na kuhimiza amani na maendeleo duniani.

Amesema, “Katika miaka 20 iliyopita, baraza hilo limefuata mwelekeo wa maendeleo ya Asia na nchi zilizoibuka kiuchumi, na kutoa sauti na mipango kwa ajili ya maendeleo ya Asia.

Pia limeimarisha nia ya kufungua mlango na kupata mafanikio ya pamoja, kulinda utekelezaji wa utaratibu wa pande nyingi, na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kufanya kazi ya kiini.”

Kwenye mkutano huo, kongamano la wanaviwanda vya China na Marekani pia limefanyika kama zamani. Bw. Li amesema pande hizo mbili zimejadili namna ya kuondoa mvutano wa kibiashara, kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kuhimiza uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili kuendelea vizuri. Amesema wanaviwanda wa nchi hizo wote wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano. CRI

  • Tags

You can share this post!

MKU yashirikiana na KFS kutekeleza miradi ya upanzi wa miti

Messi afunga mabao mawili na kuongoza Barcelona kupepeta...