Kukubo, aliyeshika mkia 2007, atangaza kuwania urais tena Agosti 9

Kukubo, aliyeshika mkia 2007, atangaza kuwania urais tena Agosti 9

Na BRIAN OJAMAA

MGOMBEA urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa 2007, Bw Nixon Kukubo, ametangaza kwa mara nyingine kuwania wadhifa uo huo katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Bw Kukubo amesema kuwa atawania kama mgombea huru huku akielezea matumaini ya kumbwaga kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, kiongozi wa UDA Naibu Rais William Ruto na Musalia Mudavadi na kuibuka rais.

Mwanasiasa huyo alikung’uta mkia kwa kura 5,927 katika uchaguzi mkuu wa 2007 ambapo rais mstaafu Mwai Kibaki alitangazwa mshindi. Bw Odinga pia alishiriki uchaguzi huo.

Bw Kukubo amesema yuko pazuri katika katika uchaguzi ujao na atawashinda kwa mbali wagombea wengine atakaomenyana nao.

“Kutokana na tajriba yangu kuu kisiasa ninaamini kwamba ninatosha kuongoza Kenya katika uchaguzi ujao na kulikomboa taifa hili linaloendelea kuzama kutokana na uongozi duni,” alisema.

Alisema kuwa wakati umewadia kwa taifa hili kuwa na kiongozi aliyemakinika na atakayetilia maanani maslahi ya wapigakura.

Aidha, alishambulia vikali viongozi wa Azimio la Umoja na ‘Earthquake’ akisema hawafai kuongoza taifa hili.

You can share this post!

Karua aanza mikutano ya kuvumisha Narc-K tayari kwa...

Balotelli atafaulu kuchezea Italia tena?

T L