KAULI YA WALLAH BIN WALLAH: Kukuza na kuendeleza Kiswahili ni dhima yetu sisi sote ulimwenguni

KAULI YA WALLAH BIN WALLAH: Kukuza na kuendeleza Kiswahili ni dhima yetu sisi sote ulimwenguni

Na WALLAH BIN WALLAH

KATIKA uwanja wa kandanda refarii hachezi lakini wajibu wake mkubwa ni kuchezesha mpira na kudhibiti nidhamu na kanuni za mchezo uwanjani.

Naye kocha au mkurufunzi huwafunza na kuwahimiza wachezaji.

Shuleni wajibu wa mwalimu ni kufundisha na kutoa maelekezo ambayo wanafunzi wakizingatia na kutekeleza, watafanikisha sana matokeo ya mtihani wao!

Muhimu ni utekelezaji!Juma lililopita mnamo tarehe 23/11/2021 tulitangaziwa rasmi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa, Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwamba tarehe saba Julai kila mwaka itakuwa siku maalum ya kuadhimisha Lugha ya Kiswahili ulimwenguni.

Baada ya tangazo hilo kuvuma na kuzagaa ulimwenguni kote, wanahabari nchini na kimataifa wakiwamo: Victor Mulama wa Redio Maisha Kenya, Khamisi Darwesh wa Redio China, Benson Wakoli na Ali Bilali wa Redio Ufaransa walinitafuta kunihoji nitoe maoni kuhusu umuhimu na jinsi tangazo hilo la UNESCO litakavyochangia kuchochea ari na harakati za kukuza na kuendeleza Kiswahili nchini na ulimwenguni!

Ndugu wapenzi, UNESCO ni kama refarii!

Sisi watumiaji wa Kiswahili ndio wachezaji uwanjani!

Tangazo la UNESCO ni kipenga kilichopulizwa!

Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno!

Tujiandae kuyatekeleza maadhimisho ya kwanza ya Kiswahili 07/07/2022 pale WASTA!

You can share this post!

KAULI YA MATUNDURA: Mapema mno kusherehekea mchakato wa...

Riziki: Wamlilia Ruto awatoe kwa ukahaba

T L