Kuna pilipili mboga za rangi tofauti, kila moja ina faida yake mwilini

Kuna pilipili mboga za rangi tofauti, kila moja ina faida yake mwilini

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

WENGI wetu tunafahamu kuwa pilipili mboga ni kiungo cha mboga katika mapishi mbalimbali, lakini hatufahamu kwamba ni miongoni mwa mboga zenye vitamini nyingi, achilia mbali uwezo wa kuboresha mifumo ya mwili.

Pilipili rangi ya njano ndio mboga pekee yenye zeaxanthin kwa wingi kuliko mboga yoyote ikifuatiwa na mahindi yanayoshika nafasi ya pili.

Pilipili mboga ina uwezo wa kuongeza kinga ya mwili pamoja na kupambana na magonjwa ya saratani na moyo, huku ikisaidia kuboresha uwezo wa macho kuona vizuri.

Mbali na kuwa kiungo kutumika katika mboga ua kachumbari na wakati mwingine hutumika kama saladi.

Pilipili mboga hutumika kwa kutengeneza juisi ambayo husaidia kutoa taka mwilini.

Pilipili mboga hupatikana katika mwonekano wa rangi tofauti ambazo ni rangi nyekundu, kijani, urujuani na njano na zinatajwa kuwa mboga yenye vitamin zaidi ya 30.

Miongoni mwa faida zilizopo katika pilipili mboga ni kwamba hutibu hali ya mtu kuwashwa na koo na pia vidonda vilivyopo kooni.

Ni muhimu pia kwa watu wanaotokwa damu puani na huimarisha kinga ya mwili kutokana na wingi wa vitamini C iliyopo ndani ya kiungo hicho ambacho hupigana dhidi ya magonjwa na kujenga kinga imara.

Pilipili mboga husaidia watu wenye shida katika mfumo wa upumuaji kutokana na kuwa na vitamini C nyingi, hukinga dhidi ya magonjwa ya kansa ya kibofu cha mkojo na ugonjwa wa baridi yabisi.

Husaidia kupunguza uzani, kuboresha mzunguko wa damu na kupunguza lehemu mwilini kwa sababu ina kiwango kidogo cha kalori na pia huzuia shinikizo la damu na kutibu anemia.

Hutibu kuhara, ugonjwa wa homa ya manjano, hurekebisha presha ya kupanda na husaidia katika kuhakikisha mmeng’enyo wa chakula unafanyika vizuri.

Wale wanaosumbuliwa na gesi tumboni wanashauriwa kutengeneza juisi ya pilipili mboga wakichanganya na juisi ya spinachi.

Pilipili mboga ya rangi ya njano ikitumika vizuri katika mapishi, ni mboga yenye faida nyingi kiafya bila kutaja ladha ya kipekee! Ina uwezo mkubwa wa kuboresha mifumo mbalimbali mwilini.

Wataalamu wa masuala ya afya wanasema pilipili mboga ya rangi ya njano ni chanzo kizuri cha virutubisho aina ya lutein na zeaxanthin ambayo huzuia matatizo ya mtoto wa jicho na udhaifu wa misuli.

Pilipili mboga rangi nyekundu (red pepper) inabaki kuwa mojawapo ya vyakula vichache vyenye kirutubisho cha lycopene ambacho hupunguza hatari ya saratani mbalimbali.

You can share this post!

Uhuru mbioni kufufua Nasa

Mwanasiasa mkongwe George Nthenge afariki