Kunguni waongezeka katika lojing’i Kisumu

Kunguni waongezeka katika lojing’i Kisumu

Na RUSHDIE OUDIA

SERIKALI ya Kaunti ya Kisumu imetishia kufunga lojing’i na hoteli zote ikiwa hazitachukua hatua ya kukabiliana na kunguni waliovamia majengo yao.

Hii ni kufuatia malalamishi kutoka kwa wakazi na wasafiri kuhusu ongezeko la kunguni wanaowahangaisha usiku kucha katika lojing’i moja almaarufu Yurop.

Baadhi ya wapenda burudani wanaopanga makazi Yurop kwa shughuli za ziada wamelalamika kuwa sasa wanalazimika kupambana na kikosi cha kunguni hao waliovamia vyumba hivyo.

Maeneo mengine yaliyovamiwa na kunguni ni shule za mabweni, makazi na vilevile kwenye matatu.

“Idara inayosimamia Huduma ya Afya ilifanya ukaguzi na kugundua kwamba kuna ongezeko kubwa la mbu, kunguni, panya na wadudu wengineo kwenye hoteli, lojing’i na maeneo mengine ya makazi Kisumu,” alisema Msimamizi wa Mji wa Kisumu, Bw Abala Wanga.

  • Tags

You can share this post!

TAMTHILIA: Mtiririko wa matukio katika Sehemu ya I, Onyesho...

PAC yatisha kukatiza pesa za mashirika, wizara ambazo wakuu...

T L