Kura: Raila amlemea Dkt Ruto nyumbani kwa Munya

Kura: Raila amlemea Dkt Ruto nyumbani kwa Munya

NA DAVID MUCHUI

WAZIRI wa Kilimo Peter Munya amedhihirisha vyema uungaji mkono wake kwa kinara wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Raila Odinga, baada ya kuhakikisha kiongozi huyo anamshinda Naibu Rais Dkt William Ruto katika kituo chake cha kupiga kura cha Ncuui, Tigania Mashariki.

Bw Odinga alipata kura 434 dhidi ya 218 za Dkt Ruto katika kituo hicho ambapo Bw Munya alipiga kura yake.

Mwaniaji wa Roots, Profesa George Wajackoya, naye alipata kura tatu kituoni humo.

Isitoshe, katika kituo cha soko la Muthara ambalo liko kilomita moja kutoka nyumbani kwa Bw Munya, Bw Odinga alipata kura 320 huku Dkt Ruto akipata 308.

Bw Munya aliandaa mkutano wake wa mwisho wa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu katika soko la Muthara wiki jana, ambapo alirai wakazi wa eneo pana la Mlima Kenya wamuunge mkono Bw Odinga ili kumuokoa kisiasa.

Pia aliwataka wakazi wamchague aliyekuwa mbunge Mpuru Aburi ambaye analenga kiti hicho kupitia chama cha NOPEU, ambacho pia kiko katika muungano wa Azimio.

  • Tags

You can share this post!

Washirika wa Uhuru waangushwa na Ruto

Bedzimba avunja ‘mkosi’ akipewa fursa tena Kisauni

T L