Kura za Bobi Wine zaongezeka

Kura za Bobi Wine zaongezeka

DAILY MONITOR NA WANGU KANURI

MPINZANI wa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa urais nchini Uganda Bobi Wine ameonekana kujizolea kura nyingi zaidi katika hesabu zilizotolewa Jumamosi asubuhi, ingawa Bw Museveni angali kifua mbele.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, Simon Byabakama amesema kuwa kura Bobi Wine sasa zimeongezeka na kufika 3,119,965 ambazo ni asilimia 34.62 ya kura zote.

Waakati huo huo, asilimia ya kura za Bw Museveni ilipungua kutoka 61.98 hadi 58.83, katika uchaguzi ambapo Waganda zaidi ya milioni 9 walijitokeza kupiga kura.

Hii ni mara ya kwanza kwa kura za Bw Museveni kushuka na kufika chini ya asilimia 60, tangu kura zianze kuhesabiwa hapo Alhamisi katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura cha Kyambogo, Kampala.

Hata hivyo, ikiwa Bw Museveni atadumisha uongozi kwa asilimia ya zaidi ya 50, ataweza kuibuka mshindi na kuendeleza utawala wake hadi miaka 40.

Kulingana na matokeo ya muda, Bw Museveni anaongoza kwa kura 5,303,831 za kura 9,100,865 halali.

Matokeo hayo ni kutoka vituo 30,098 kati ya 34,684, yakiwa asilimia 86.78 ya kura zote yaliyotolewa Jumamosi saa tatu asubuhi.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Waandamanaji wa Amerika na wa Kenya ni...

Boit, Kandie kujaribu kubwaga Cheptegei na Mo Farah Olimpiki