Kimataifa

Kuua wanawake 5 kulinifanya nijihisi mkamilifu, asema mwanaume

February 5th, 2019 2 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAUME aliyefungwa kwa kuwaua wanawake watano wa umri mdogo, wakiwemo watoto wawili wa miaka 14 baada ya kuwabaka alieleza shirika moja la habari kuwa alihisi vyema kila alipoua mwanamke wa umri mdogo.

Bw Bernard Giles alieleza shirika hilo kuwa lengo lake maishani lilikuwa kuwaua wanawake wa umri mdogo, ndipo ahisi mkamilifu. Alikiri kuwa alitekeleza mauaji hayo bila kusita.

Alisema kuwa kila mauaji aliyotekeleza yalipokuwa yakizungumziwa, alihisi vyema na kujihisi kuwa aliye juu ajabu.

Giles anaenda kwenye kumbukumbu za Marekani ka mmoja wa wauaji wasumbufu na hatari zaidi. Alianza tabia hiyo awali miaka ya ’70, alipotekeleza mauaji ya kikatili zaidi kuwahi kushuhudiwa.

Wadhulumiwa wake walikuwa wanawake wa umri mdogo waliokuwa wakizuru kujiburudisha maeneo tofauti na aliwateka nyara kisha kuwabeba kwa gari akiwa na bunduki hadi kati ya misitu, ambapo aliwadhulumu kingono kabla ya kuwaua.

Wanwake hao walikuwa Paula Hamric wa miaka 22 na ambaye alikuwa mama wa watoto wawili, Nancy Gerry wa miaka 18, Carolyn Bennett wa miaka 17. Aidha, aliwaangamiza Sharon Wimer na Krista Melton, wote wa miaka 14.

Na alipoulizwa ikiwa aliwaua wanawake na watoto hao, alikiri bila kusita.

Alisema kuwa alianza tabia ya kuua alipokuwa na miaka 20, alipokuwa akifanya kazi katika kampuni ya umeme.

Wakati huo kabla hajaanza vituko hivyo alikuwa katika ndoa na mwanamke wa miaka 18 Leslie, ambapo walijaliwa na mtoto msichana, kwa jina Heather.

Alifichua kuwa alibaini kuwa alikuwa na hamu ya kutekeleza mauaji alipokuwa na umri wa miaka sita.

Alisema kuwa wakati huo walipokuwa wakicheza mchezo wa kujificha na watoto wenzake, alikumbana na mtoto msichana katika chumba cha kulala ambapo hapakuwa na mtu na akamwangusha chini.

“Nakumbuka nikimlalia na kumlalia tulipokuwa tukicheza… hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu,” akasema.

“Kutoka wakati huo, kila kitu nilichoona ama kusoma kilikuwa na kitu kuhusiana na dhuluma za kingono dhidi ya mwanamke. Nilipokuwa nikikua, nilianza kutaka sana kujua kuhusu suala hilo la dhuluma za ngono dhidi ya mwanamke.”

Alieleza kuwa kila alipotaka kudhulumu na kuua mwanamke, mbinu aliyotumia ni kumfikia.

Alisema kuwa hata hakumbuki majina ya wale aliowaua, kwani aliwachukulia kama vitu tu ila si watu.