KVF yafanyia timu za taifa za Kenya mabadiliko 11 zikianza matayarisho ya Kombe la Afrika

KVF yafanyia timu za taifa za Kenya mabadiliko 11 zikianza matayarisho ya Kombe la Afrika

Na AGNES MAKHANDIA

SETA mzoefu wa Kenya Prisons Daniel Kiptoo ni miongoni mwa wachezaji saba wapya katika kikosi cha timu ya wanaume ya Kenya kilichotajwa kujiandaa kwa Kombe la Afrika litakalofanyia Septemba 5-15 jijini Kigali, Rwanda.

Wachezaji wengine wapya katika kikosi cha kocha Gideon Tarus ni washambuliaji Peter Kamara (KPA), Meshack Wambua (Kenya Prisons), Michael Chemos (Kenya Prisons), mzuiaji wa kati Rodgers Kipkirui (Kenya Prisons) na libero kutoka GSU Noah Bett pamoja na mchezaji wa kati Naftali Chumba.

Kiptoo pamoja na Kamara, Wambua, Kipkirui, Chumba, Chemos na Bett ambaye mara ya mwisho alichezea Kenya ni mwaka 2015, hawakuwa katika kikosi cha kwanza kilichotajwa juma lililopita.

Kiptoo amejaza nafasi ya mchezaji mwenza Kelvin Kipkosgei ambaye ametemwa.

Kiptoo, ambaye aling’ara katika mashindano ya timu nne-bora ya kuamua mshindi wa Ligi Kuu yaliyokamilika Agosti 29 jijini Mombasa, ametaka wachezaji wenzake wajitolee kwa dhati mazoezini na kwenye mashindano hayo.

“Tuna kikosi kizuri, na kutokana na kushiriki kwetu katika mashindano ya timu nne-bora, tuko tayari kwa mashindano ambacho ni kitu kizuri kwetu,” alisema Kiptoo.

Akitaja vikosi vya kuanza mazoezi baada ya ligi kutamatika katika ukumbi wa KPA Makande, mwenyekiti wa kwanza na kiongozi wa msafara wa timu ya Kenya inayoenda Rwanda, Charles Nyaberi, alisema kuwa wachezaji 18 wataingia kambini Agosti 30 ugani Nyayo. Nahodha wa timu hiyo ya wanaume ni Jairus Kipkosgei.

Libero wa Equity Bank James Mutero na mshambuliaji Kevin Kevin Omuse wametemwa.

Tarus, ambaye timu yake ya GSU ilihifadhi ufalme wa Ligi Kuu ya wanaume wikendi, alisema kuwa muda uliosalia kabla ya mashindano ni mchache kwa hivyo watamakinikia tu mfumo kabla ya mashindano hayo ya siku 10 ambayo timu mbili za kwanza zitaingia mashindano ya dunia.

Katika kikosi cha kinadada, mchezaji anayetumia mkono wa kushoto Violet Makuto alipuuza mwito kwa kujiunga na timu ya taifa baada ya kupata jeraha la mguu.

Makuto alitemwa kabla ya Malkia Strikers kuelekea jijini Tokyo nchini Japan kwa michezo ya Olimpiki. Amesema anataka kupona kabisa kabla ya kurejea ulingoni msimu ujao.

Nafasi ya mchezaji huyo kutoka klabu ya KCB imechukuliwa na Anne Lowen kutoka Kenya Prisons. Wachezaji wa klabu ya DCI, Veronica Adhiambo na Josphine Wafula wataanza mazoezi Jumatano. Seta wa Kenya Pipeline Esther Mutinda, ambaye alijiondoa kabla ya Olimpiki, amerejeshwa kikosini. Kombe la Afrika la kinadada ni Septemba 10-20 jijini Kigali.

Kikosi cha kinadada cha Malkia Strikers kuanza mazoezi:

Jane Wacu, Joy Lusenaka, Esther Mutinda, Edith Wisa, Lorine Chebet, Gladys Ekaru, Yvonne Sinaida, Ann Lowem, Mercy Moim, Leonida Kasaya, Noel Murambi, Meldin Sande, Veronica Adhiambo, Agripina Kundu, Elizabeth Wanyama, Josephine Wafula, Sharon Chepchumba na Emmaculate Chemutai.

Maafisa – Kocha Mkuu Paul Bitok, kocha msaidizi Japheth Munala, kocha wa pili msaidizi Josp Barasa, msaidizi katika mazoezi Esther Jepkosgei, ‘chaperone’ Emily Mbotela, meneja wa timu David Kilundo na kiongozi wa msafara Charles Nyaberi.

Kikosi cha wanaume cha kuanza mazoezi: Simon Kipkorir, Cornelius Kiplagat, Naftali Chumba, Brian Melly, Nelson Bitok, Rodgers Kipkirui, Lennis Ochieng, Bernard Wechuli, Peter Kamara, Alphas Makuto, Enock Mogeni, Cornelius Kiplagat, Dennis Omollo, Michael Chemos, Naftali Chumba, Aggrey Kibungei, Meshack Wambua, Brian Melly, Daniel Kiptoo, Sam Juma na Noah Bett. Maafisa – kocha mkuu Gideon Tarus, msaidizi David Lung’aho, kocha wa pili msaidizi Sammy Mulinge, msaidizi wa mazoezi Elisha Aliwa na meneja wa timu Kenneth Tonui. TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

LEONARD ONYANGO: Wakuu wa shule waliotafuna mabilioni...

Messi achezea PSG kwa mara ya kwanza