Makala

KWA KIFUPI: Maambukizi yanayosababisha vidonda baridi au malengelenge

August 6th, 2019 1 min read

Na PAULINE ONGAJI

‘HERPES’ ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na virusi vya Herpes Simplex Virus (HSV).

Virusi hivi huathiri sehemu ya nje ya nyeti, sehemu ya tupu ya nyuma (anus), utando wa kamasi na ngozi katika sehemu zingine za mwili.

Hii ni hali ya kudumu, japo kuna baadhi ya watu ambao huenda wasiwahi kuonyesha dalili za maradhi haya licha ya kuwa na virusi hivi.

Husababishwa kwa kugusana moja kwa moja na viowevu vya mwili au vidonda vya mtu aliyeambukizwa.

Kuenea bado kunaweza kutokea hata iwapo dalili hazipo.

Maambukizi yaweza kufanyika kwa kushiriki tendo la ndoa bila kinga, kushiriki ngono ya mdomoni na mtu ambaye hukumbwa na vidonda vya mafua, kutumia vidude vya ngono kwa pamoja, sehemu za siri kushikana na mtu za aliyeambukizwa.

Yanaweza kuenezwa kwa mtoto mchanga wakati wa kuzaliwa pia.

Ishara

Ishara za maradhi haya ni pamoja na malengelenge, vidonda, maumivu unapokojoa, vidonda vinavyoambatana na mafua na kutokwa kwa majimaji ukeni.

Tiba na kinga

Japo mgonjwa hawezi kupona, kuna tiba kupitia dawa utakazohitajika kutumia kila siku kudhibiti virusi na kupunguza makali.

Matumizi ya kondomu yanaweza kupunguza maambukizi ila si kuondoa hatari.

Kutumia kondomu, na vitulizo vya kawaida nyumbani.

Hakuna chanjo inayopatikana kuzuia maambukizi.