Michezo

KWAHERI KOBE: Majonzi dunia nzima

January 27th, 2020 2 min read

Na MASHIRIKA

LOS ANGELES, Amerika

UCHUNGUZI wa kina unaedelea kubaini kilichosababisha ajali ya helikopta iliyowaua watu tisa Jumapili, akiwemo nyota wa mpira wa vikapu nchini Amerika, Kobe Bryant na binti yake Gianna Maria-Onore Bryant aliyekumbana na mauti akiwa na umri wa miaka 13.

Bryant anayetambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa vikapu, alikuwa bingwa mara tano wa ligi kuu ya vikapu nchini Amerika (NBA) na pia mshindi wa Oscar.

Marehemu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 41, alikuwa anasafiri kwa ndege kibinafsi ambayo ilianguka na kuwaka moto katika eneo la Calabasas, California, kutokana na hali mbaya ya anga.

Wengine walioangamia ni kocha wa Orange Coast College (OCC), John Altobelli, mkewe Keri, mtoto wao, Ayssa, nduguye Altobelli aliwaambia waandishi. Alyssa na Gianna walikuwa wakichezea timu moja, naibu kocha wa OCC, Ron La Ruffa alisema jana.

Ilikuwa kawaida kwa Altobeli kusafiri na bintiye wakati wa mechi, La Ruffa aliiongeza.

“Kama jamii ya OCC tumempoteza mtu muhimu, na hivi sasa tunaomboleza kwa uchungu mwingi,” alisema Rais wa OCC, Angelica Suarez kwenye taarifa. “Kocha Altobelli alikuwa mtu muhimu katika taasisi hii, mwalimu aliyeheshimiwa, kocha na rafiki mkubwa. Huu ni mkaza mkubwa kwa jamii yetu.”

Kadhalika imethibitika kwamba Christina Mauser ambaye ni naibu kocha wa timu ya wasichana katika shule ya binafsi ya Corona de Mar ni miongoni mwa waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo.

“Watoto wangu na mimi binafsi tumeshtuka mno. Nimepoteza mke wangu, na pia watoto wamepoteza mama yao mpendwa,” Matt Mauser aliandika kwenye mtandao wake wa binafsi.

Mkuu wa polisi wa Los Angeles anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika kwenye ajali hiyo iliyotokea majira ya asubuhi, saa za Amerika.

Afisa Mkuu wa Afya wa Kaunti ya Los Angeles, Jonathan Lucas alisema wamekumbwa na wakati mgumu kufikia miili hiyo, huku akiongeza kwamba wanashirikiana na mashirika mengine ya uchukuzi nchi kafu na angali katika shughuli hiyo.

Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.

Vile vile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa michezo ya Olimpiki.

Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya

Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.

Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wakike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.

Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19-aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo, na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.

Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.

Ingawa baadae aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.

Salamu nyingi za rambirambi zimemiminika katika mitandao ya kijamii kufatiwa taarifa ya ajali hiyo.

Shaquille O’Neal ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004,alisema kuwa hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu ambayo anayo.

“Ninakupenda na utakumbukwa,” aliandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.

Deron Williams, alikuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olympiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. Alimuelezea Bryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.