Kwangu 2022 umekuwa mwaka wenye mafanikio makubwa – Nyota Okutoyi

Kwangu 2022 umekuwa mwaka wenye mafanikio makubwa – Nyota Okutoyi

NA GEOFFREY ANENE

MWANATENISI Angella Okutoyi ameelezea kufurahishwa na jinsi mwaka 2022 umemwendea.

Akizungumza na Taifa Spoti baada ya kuwasili nyumbani jana kutoka Amerika, Okutoyi alisema sasa anatupia jicho mashindano ya wanawake ya dola 15,000 za Amerika (W15) jijini Nairobi.

Angella Okutoyi alipopigwa picha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) mnamo Septemba 19, 2022 akiwa na taji la J1 Repentigny alilotwaa kwa kushirikiana na Malwina Rowinska nchini Canada kabla ya mashindano ya US Open kwa upande wa chipukizi. PICHA | GEOFFREY ANENE

“Nimepata matokeo mazuri na pia mengine yasiyo mazuri, lakini kwa jumla umekuwa mwaka mzuri kwangu tangu Januari. Nimepata mafanikio na uzoefu katika mechi za mchezaji mmoja kila upande na pia wachezaji wawili kila upande,” alitanguliza.

“Nafurahia kwa nafasi yangu nzuri kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF), nambari 49. Niko ndani ya 50-bora ambayo ndio nafasi yangu nzuri kabisa,” aliongeza Okutoyi.

Angella Okutoyi (kati) akiwa na Katibu Mkuu wa Tennis Kenya Wanjiru Mbugua (kushoto) na kocha Rosemary Owino katika uwanja wa JKIA jijini Nairobi mnamo Septemba 19, 2022. PICHA | GEOFFREY ANENE

Mkenya huyo alifika raundi ya tatu kwenye Grand Slam ya haiba ya chipukizi nchini Australia, raundi ya pili ya French Open, kushinda taji la wachezaji wawili Wimbledon na kufika raundi ya pili ya mchezaji mmoja na wachezaji wawili US Open.

Katibu wa Shirikisho la Tenisi Kenya, Wanjiru Mbugua, alisema ni furaha kuwa Okutoyi ameitiwa ufadhili wa katika taasisi za elimu ya juu nchini Amerika.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Kaunti zina jukumu kubwa kuzima njaa

Sikuona Moi akiuza shamba – Wakili

T L