Kylian Mbappe aongoza PSG kupepeta Nice na kudhibiti kilele cha jedwali la Ligi Kuu ya Ufaransa

Kylian Mbappe aongoza PSG kupepeta Nice na kudhibiti kilele cha jedwali la Ligi Kuu ya Ufaransa

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe alitokea benchi na kufungia Paris Saint-Germain (PSG) bao la pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Nice katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Lionel Messi alifungulia PSG ukurasa wa mabao kabla ya Nice kusawazisha kupitia kwa Gaetan Laborde.

PSG hawajapoteza mchuano wowote chini ya Christophe Galtier – kocha wa zamani wa Nice aliyemrithi Mauricio Pochettino ugani Parc des Princes mnamo Julai.

Miamba hao wanadhibiti sasa kilele cha jedwali la Ligue 1 kwa alama 25, mbili kuliko nambari mbili Olympique Marseille waliokung’uta Angers 3-0. PSG wameshinda mechi nane na kutoka sare mara moja katika mechi tisa zilizopita ligini.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Jumamosi):

PSG 2-1 Nice

Strasbourg 1-3 Rennes

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

AS Roma ya kocha Jose Mourinho yazamisha chombo cha Inter...

Erling Haaland aongoza Man-City kupepeta Man-United 6-3...

T L