Kylian Mbappe asema angali na ndoto ya kuchezea Real Madrid katika siku za usoni

Kylian Mbappe asema angali na ndoto ya kuchezea Real Madrid katika siku za usoni

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe amesema ndoto ya kuchezea Real Madrid katika siku za usoni haijazimika licha ya maamuzi yake ya kupuuza ofa ya miamba hao wa Uhispania na kurefusha mkataba kambini mwa Paris Saint-Germain (PSG).

Mbappe, 23, alitia saini kandarasi mpya ya miaka mitatu katika kikosi cha PSG mnamo Mei 21, 2022. Hata hivyo, ameshikilia kwamba angali na azma ya kuchezea Real baadaye katika safari yake ya kitaaluma.

“Huwezi kujua kitakachofanyika katika siku za halafu. Hata hivyo, nafikiria zaidi kuhusu ya sasa kwa kuwa ningali mchezaji wa PSG kwa miaka mingine mitatu ijayo,” akasema.

“Ingawa nimerefusha muda wa kuhudumu kwangu PSG, ndoto ya kuvalia jezi za Real hapo baadaye hazijazimika,” akaongeza Mbappe kwa kufichua kwamba alizungumza moja kwa moja na rais wa Real, Florentino Perez kuhusu uamuzi wake wa kusalia PSG.

Nyota huyo wa zamani wa AS Monaco nchini Ufaransa, alifungia PSG mabao 28 msimu huu na kuongoza miamba hao kutwaa taji la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Alijiunga na PSG mnamo 2017 na ameongoza kikosi hicho kunyanyua mataji manne ya Ligue 1 na matatu ya French Cup.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Sonko aanza kusuasua

Kwekwe kuendelea kumpigia debe Boga

T L