Makala

La hasha, Nyambaria High haijapata A tupu mara hii, Knec yafafanua

January 9th, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

BARAZA la Kitaifa la Mtihani Nchini (KNEC) limekanusha madai yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa shule ya wavulana ya Nyambaria imezoa alama ya A.

Shule hiyo iliyoko Kaunti ya Nyamira ina wanafunzi zaidi ya 2,500.

Mwaka wa 2022  wanafunzi 383 walipata alama ya A- huku wanafunzi 76 wakipata alama ya B+  na mwanafunzi mmoja akipata alama ya B.

Kupitia ukurasa wa X ambao awali ulifahamika kama Twittter, Baraza la Mtihani nchini lilitoa taarifa rasmi kwenye mitandao ya kijamii, na kusema habari za Nyambaria High kupata alama ya A kuwa ni feki.  Lilisisitiza umuhimu wa kuthibitisha habari kabla ya kusambaza.

“Habari ghushi,” ilipakia mtandaoni.

Mitandao ya Kijamii, wanamitandao walisambaza picha moja, iliyokuwa na ujumbe kuwa shule hiyo ilipata Alama ya A katika matokeo ya KCSE.

Matokeo hayo yalionyesha uwezekano wa kutiliwa shaka kwa kusajili alama ya A kwa wanafunzi wote.

Habari hiyo ilisambaa kwa haraka mitandaoni na kusababisha sintofahamu miongoni mwa watumiaji wa mitandao kuhusu mafanikio ambayo hayajawahi kushuhudiwa.

Kwenye picha hiyo iliyokuwa ikisambaa iliibua maswali kuhusu maadili ya mfumo wa Mitihani na uwezekano wa kutokea kwa aina hiyo katika mtihani.

Novemba 8, 2023, mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Onyari ambaye alikuwa maneja wa kituo cha mtihani, alisimamishwa kazi kutokana na madai ya udanyanyifu wa mitihani.