Laikipia yalipia makosa ya Wakoloni

Laikipia yalipia makosa ya Wakoloni

Na JOHN KAMAU

MAKABILIANO yanayoendelea katika Kaunti ya Laikipia na kutajwa kama ujangili yanatokana na makosa ya kihistoria ambapo miaka 110 iliyopita, wakoloni walilazimisha jamii ya Wamaasai kuacha maeneo waliyokuwa wakilisha mifugo yao.

Katika kile ambacho jaji mmoja wa kikoloni aliidhinisha kama mkataba kati ya nchi mbili, Laikipia iligeuka kuwa uwanja wa vita hasa wakati wa kiangazi.

Wakati huu, eneo hilo limebaki kukabiliana na athari za unyakuaji ardhi ulioanzishwa na mlowezi aliyejulikana kama Sir Charles Eliot.

Msingi alioweka mtawala huyo wa kikoloni umefanya vigumu kwa matatizo ya ardhi Laikipia kutatuliwa kwa kutumia polisi inavyojaribu kufanya serikali.

Ili kupatia masettla wazungu mashamba, serikali ya wakoloni chini ya Sir Charles, iliunda njama ya kufukuza Wamaasai katika moja ya uhamisho mkubwa zaidi wa jamii nchini wakati huo.

Ukweli ni kwamba, kama angeruhusiwa, Sir Charles angekuwa amefanya mabaya zaidi. Kulingana na stakabadhi aliyoandika Oktoba 24 1963, mlowezi huyo alianika mipango yake kwa kusema:

“Hakuna shaka kwamba, Wamaasai na makabila mengine makubwa lazima yaishe. Ni jambo ninalotazamia. Sina hamu ya kulinda ufalme wa Wamaasai, ukipotea haraka iwezekanavyo na isijulikane, isipokuwa katika vitabu vya kumbukumbu za kale, itakuwa bora zaidi.”

Eliot aliamini katika msingi wa wakoloni wazungu, sawa na ilivyokuwa ikifanyika Afrika Kusini na alishikilia kuwa “eneo la ndani la koloni lilikuwa nchi ya mtu mweupe.”

Malisho

Laikipia ilikuwa eneo la mwisho la wakoloni Kenya. Ardhi yake nzuri ya malisho, mito na vijito sasa inapatikana ndani ya ardhi ya kibinafsi.

Huku maeneo ya malisho yakiendelea kupungua na mabadiliko ya tabia nchi kuendelea kupatia wafugaji changamoto kwa shughuli zao za kiuchumi, mashamba ya kibinafsi yataendelea kulengwa.

Hili bila shaka sio suala litakalotatuliwa haraka.

Sir Charles, pamoja na hatua alizochukua alikuwa ameonywa kuhusu hatari ya kupokonya Wamaasai na Wakikuyu kutoka Kiambu ardhi yao na akaendelea kufanya hivyo hadi kashfa ilipoibuka kuhusu kampuni ya uchimbaji madini ambayo ilikuwa imenyakua ardhi kubwa.

Alilazimika kujiuzulu lakini uharibifu tayari ulikuwa umefanyika. Alikuwa ameweka msingi wa mkataba wa kwanza wa Wamaasai wa 1904 ambao alikuwa amebuni Laikipia kuwa mali ya Wamaasai pamoja na eneo la kusini waliloita Southern Reserve.

Ilikuwa ni mrithi wake, Sir Donald Stewart, ambaye alitia saini mkataba wa kwanza wa Wamaasai

You can share this post!

Corona yachangia wanafunzi 400,000 kukatiza masomo

Mpinzani mkuu wa Kagame akamatwa kwa dai la unajisi