Lenku apigwa jeki wazee wa Agikuyu wakiunga azma ya kutetea wadhifa

Lenku apigwa jeki wazee wa Agikuyu wakiunga azma ya kutetea wadhifa

NA STANLEY NGOTHO

AZMA ya Gavana wa Kajiado, Joseph Ole Lenku kutetea wadhifa wake, Jumapili ilipigwa jeki baada ya Baraza la Wazee wa Agikuyu kutangaza kuwa watamuunga mkono kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 2022.

Wanachama hao wa Kiama Ki Ma, walisema kuwa gavana huyo, amesaidia kueneza amani na kuhakikisha kuna utangamano kati ya jamii mbalimbali zinazoishi eneo hilo na katika uteuzi, hakubagua jamii yoyote.

Mwenyekiti wao, Bw Igecha Waithaka, pamoja na wazee hao waliovalia mavazi ya kitamaduni, walimwombea Bw Lenku katika eneo la kufanya tambiko huko Lekuruki, Kajiado Kaskazini.

  • Tags

You can share this post!

Wetang’ula sasa ataka Raila akamatwe

Hofu Mlimani kuhusu unaibu rais

T L