Leon Goretzka na Declan Rice kati ya wanasoka 5 wanaoviziwa sasa na Man-United

Leon Goretzka na Declan Rice kati ya wanasoka 5 wanaoviziwa sasa na Man-United

Na MASHIRIKA

SIKU moja baada ya kuafikiana na Borussia Dortmund kuhusu uhamisho wa kiungo mvamizi Jadon Sancho kutoka ugani Signal Iduna Park hadi Old Trafford, Manchester United wamefichua mpango wa kuendelea kujisuka zaidi kwa ajili ya msimu mpya wa 2021-22.

Kwa mujibu wa kocha Ole Gunnar Solskjaer, kubwa zaidi katika maazimio ya Man-United kwa sasa ni kusajili wanasoka watano zaidi wakiwemo Leon Goretzka wa Bayern Munich, Declan Rice wa West Ham United, Pau Torres wa Villarreal na fowadi Harry Kane ambaye pia anawaniwa na Manchester City kutoka Tottenham Hotspur.

Solskajer pia amekiri kwamba Man-United wanayahemea maarifa ya beki Kieran Trippeir wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Uingereza.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Hofu mkataba wa Kenya na Uingereza kuruhusu biashara huru...

Mawakili wakosoa hatua ya kushtaki rais