Lewandowski aongoza Bayern kukomoa Dortmund na kutwaa German Super Cup

Lewandowski aongoza Bayern kukomoa Dortmund na kutwaa German Super Cup

Na MASHIRIKA

ROBERT Lewandowski alifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake Bayern Munich kuwakomoa Borussia Dortmund 3-1 na kuhifadhi ubingwa wa taji la German Super Cup mnamo Agosti 17, 2021.

Lewandowski aliwaweka Bayern kifua mbele mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya Thomas Muller kufunga la pili dakika chache baada ya kipenga cha kuashiria mwanzo wa kipindi cha pili kupulizwa.

Ingawa Marco Reus aliwarejesha Dortmund mchezoni katika dakika ya 64 uwanjani Signal Iduna Park, Lewandowski alifungia Bayern bao la tatu katika dakika ya 74. Goli hilo lilikuwa lake la 24 dhidi ya Dortmund ambao ni waajiri wake wa zamani.

Lewandowski ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Poland, aliwahi kuchezea Dortmund kwa kipindi cha miaka minne kati ya 2010 na 2014.

Kombe la German Super Cup huwaniwa na mabingwa wa taji la Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na washikilizi wa taji la DFB-Pokal Cup. Bayern walinyakua ubingwa wa Bundesliga msimu uliopita kwa mara ya tisa mfululizo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Tammy Abraham sasa mali rasmi ya Mourinho

CECIL ODONGO: Kuna dalili uchaguzi wa 2022 huenda urudiwe