Michezo

LIgi ya Championship nchini Uingereza kurejelewa Juni 20

May 31st, 2020 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

LIGI ya Daraja la Kwanza nchini Uingereza (Championship) sasa itarejelewa mnamo Juni 20, takriban miezi mitatu baada ya kusitishwa kutokana na virusi vya homa kali ya corona.

Kwa mujibu wa vinara wa soka ya Uingereza (EFL), tarehe hiyo huenda ikabadilishwa iwapo maambukizi ya corona yatazidi au wadau watakiuka baadhi ya kanuni za afya zilizopo katika juhudi za kukabiliana na janga hilo.

Hadi kusimamishwa kwa soka ya Uingereza mnamo Machi 13, Ligi ya Championship ilikuwa na mechi 108 zaidi za kusakatwa zikiwemo za mchujo wa nusu-fainali na fainali.

Hakuna mchuano wowote wa Championship umesakatwa tangu Machi 8, 2020.