Limbukeni Brentford wawakaba Liverpool koo ligini

Limbukeni Brentford wawakaba Liverpool koo ligini

Na MASHIRIKA

YOANE Wissa alifunga bao la dakika za mwisho na kusaidia Brentford kuwalazimishia Liverpool sare ya 3-3 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumamosi ugani Community Stadium.

Goli hilo la Wissa lilisaidia Brentford kujizolea alama moja muhimu dhidi ya masogora wa kocha Jurgen Klopp waliofunga mabao yao kupitia kwa Diogo Jota, Mohamed Salah na Curtis Jones.

Chini ya kocha Thomas Frank, Ethan Pinnock aliwaweka Brentford kifua mbele katika dakika ya 27 kabla ya Vitaly Janelt kupachika wavuni goli la pili kunako dakika ya 63. Bao la Salah lilikuwa lake la 100 ligini akivalia jezi za Liverpool ambao kwa sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la EPL kwa alama 14, moja zaidi kuliko Everton, Manchester United, Chelsea na mabingwa watetezi Manchester City.

Sare iliyosajiliwa na Brentford yalisheherekewa pakubwa na kikosi hicho kilichopepetwa 4-0 na Liverpool katika mchuano wa robo-fainali ya Kombe la FA uliowakutanisha mara ya mwisho mnamo 1988-89.

Salah ndiye mwanasoka wa 13 kuwahi kufikisha mabao 100 ligini akivalia jezi za Liverpool na wa nne kufanya hivyo katika EPL baada ya Robbie Fowler, Steven Gerrard na Michael Owen.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Corona ilipunguza kasi ya mbinu za kisasa za upangaji...

Nyuki wavamia na kumuua mzee aliyehudhuria mazishi ya mjukuu