Linturi aonya wakora wanaouza mbolea ya serikali

Linturi aonya wakora wanaouza mbolea ya serikali

ERIC MATARA Na ROBERT KIPLAGAT

WAZIRI wa Kilimo Mithika Linturi amefichua kwamba wanawatumia maafisa wa Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) kupambana na wakora ambao wanapakia upya na kuuza mbolea ya serikali.

Bw Linturi alitoa ufichuzi huo wakati wa ziara yake katika kaunti za Nakuru, Bomet na Narok.

“Kuna wakora ambao wanataka kuuza mbolea ya serikali ila hatutawakubalia kamwe na DCI sasa inafuatilia suala hilo. Hatutawaruhusu wakora wateke shughuli ya kuwapa wakulima wetu mbolea,” akasema Bw Linturi akiwa Bomet.

Akiwa Narok, waziri huyo aliwahakikishia Wakenya kwamba serikali haitaagiza mahindi wakati ambapo wakulima nao watakuwa wakivuna mazao yao.

Pia aliwahakikishia Wakenya kwamba serikali imeshapata ndege pamoja na dawa za kunyunyizia ngano ili kuwaua ndege waharibifu.

  • Tags

You can share this post!

Biashara za hoteli, gesti zanoga Mokowe miaka mitatu baada...

Waandamanaji wakabiliana jijini Kisumu

T L