Makala

LISHE: Biskuti za viazi vitamu

October 14th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

Muda wa kuandaa: Dakika 30

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 5

Vinavyohitajika

  • kilo 1 unga wa ngano (self-raising)
  • vijiko 3 vya siagi; acha iyeyuke
  • chumvi
  • viazi vitamu 2 vikubwa (vichemshe kisha vipondeponde)
  • vijiko 3 vya maziwa

 

Viazi vitamu. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Chukua unga wako weka katika bakuli safi na kavu kisha washa ovena kwa moto wa nyuzi 450.

Changanya siagi, chumvi na unga. Hakikisha unachanganya vizuri.

Sasa chukua vile viazi vilivyopondwa na uchanganye katika unga pamoja na maziwa na uhakikishe inachananyika vizuri kabisa.

Kanda taratibu kwa muda wa dakika tano halafu anza kusukuma kwa kutumia mpini huu mchanganyiko wako wa unga.

Hakikisha juu ya meza unayosukumia umeweka unga wa kutosha ili mchanganyiko uweze kusukumika vizuri na usinatie kwenye meza.

Kisha kata maumbo aina yoyote upendayo.

Baada ya kukata, hakikisha unatoa miduara yako na kuiweka kando kisha unaunganisha ule unga uliobakia na kusukuma tena na unaendelea kukata kisha unarudia mpaka utakapomalizia mchanganyiko wa unga wote.

Paka mafuta katika chombo unachookea kisha ziweke biskuti juu yake na uoke katika ovena.

Oka kwa muda wa hadi dakika 25 au mpaka zitakapokuwa na rangi ya kahawia.

Zikishapoa, pakua na ufurahie.