Makala

LISHE: 'Doughnuts' za sukari ya kusaga (Icing Sugar)

August 24th, 2020 1 min read

Na MISHI GONGO

Idadi ya walaji: 8

Viungo

Unga gramu wa keki (self rising) gramu 750

sukari gramu 300

mayai 5

siagi gramu 300

iliki kiasi

‘Doughnuts’. Picha/ Mishi Gongo

Jinsi ya kutayarisha

Changanya sukari, siagi na iliki ndani ya bakuli kisha kwa kutumia mwiko au mchapo, changanya hadi vilainike.

Unga uliokandwa kama sehemu ya maandalizi ya ‘doughnuts’. Picha/ Mishi Gongo

Ongeza mayai yako endelea kukoroga hadi vichanganyike vizuri.

Ongeza unga kidogo kidogo katika mchanganyiko wako hadi mchanganyiko uwe mgumu.

Kata madonge kisha sukuma yawe ya maumbo ya duara.

Kwa kutumia chombo cha duara, kata upate umbo la gurudumu.

Bandika karai motoni halafu anza kuchoma doughnuts – donati – hadi ziwe kahawia.

Zichovye kwenye sukari ya kusaga kisha andaa.

Unaweza kuandaa kwa chai au sharubati.