LISHE: Granola

LISHE: Granola

NA MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

GRANOLA ni chakula ambacho kinaweza kutayarishwa kwa njia tofauti nyumbani.

Ni kiamsha kinywa bora chenye nafaka, matunda na karanga.

Chakula kama hicho huupa mwili nguvu na pia kusaidia katika mfumo wa umeng’enyaji.

Pia granola ni chakula chenye ladha ambacho hakihitaji kupikwa. Hii ina maana ni chakula ambacho kinaweza kuunganishwa kwa urahisi na viungo vingine kwa kuwa muundo wake wa kimsingi utatengenezwa na karanga kadhaa au hata matunda yaliyokaushwa.

Wakati mwingine tunaiona katika umbo la mpira, lakini pia inaweza kutayarishwa kwa umbo bapa. Unaweza kuila granola kama kiamshwa kinywa ukiichanyanya na yogurt au na smoothies za nyumbani.

Granola ni chanzo muhimu cha nishati kwa hiyo utaanza siku yako ukiwa mwanye nguvu. Unaitumia kwa kiamsha kinywa au kama kitafunio cha mchana. Haina protini lakini ina nyuzi nyingi, vitamini, madini na wanga ambayo hubadilishwa kuwa nishati wakati wa mchana.

Inashibisha sana na hii itakufanya uache kula vitafunio kati ya chakula, kama kawaida tunavyofanya.

Ina nyuzi nyingi na inasaida katika mmeng’enyo wa vyakula.

Ina virutubisho muhimu vinayosaidia kwa utunzaji wa ubongo, kuzuia kuzorota kwake na kuzuia magonjwa ambayo yanaweza kuwa ya kawaida ndani yake.

Granola pia ni yenye faida kwa mifupa yenye nguvu.

Kwa hivyo, ikiwa unapendelea, unaweza kuila granola kama ilivyo. Lakini ikiwa sivyo, unaweza kuongeza mtindi au matunda.

  • Tags

You can share this post!

BENSON MATHEKA: Mfumo wa usimamizi wa basari ubadilishwe...

MAPISHI KIKWETU: Saladi ya kuku, jibini na vipande vya...

T L