Habari Mseto

LISHE: Keki ya vanilla isiyo na mayai

October 16th, 2020 1 min read

NA WANGU KANURI

Jinsi ya kuandaa keki

Muda wa kuandaa: dakika kumi

Muda wa kuoka: dakika thelathini

Viungo

 • Vikombe vitatu vya unga wa ngano
 • Kikombe kimoja cha sukari
 • Kijiko nusu cha chai cha chumvi
 • Kikombe kimoja cha mafuta ya kupika
 • Viikombe viwili vya maziwa iliyoganda ama maziwa kawaida
 • Vijiko viwili vya kulia vya unga wa kuoka
 • Vijiko vinne vya chai vya vanilla
 • Kikombe kimoja cha sukari laini (icing sugar)
 • Kijiko kimoja cha chai cha maziwa
 • Chakuleti iliyoyeyuka

Maelekezo

 • Pasha tanuri yako kwa moto wa nyuzi 170.
 • Changanya unga, sukari, na chumvi pamoja. Hakikisha umechanganya vizuri.
 • Ongeza viowevu kwenye mchanganyiko wako. Viowevu hivyo ni mafuta ya kupika, maziwa
 • yaliyoganda na vanilla. Hakikisha umechanganya vizuri lakini sio sana. Mtiririko usiwe laini
 • sana.
 • Paka majarini kwenye bakuli ya kuokea kisha umimine mchanganyiko huo kwenye bakuli hiyo.
 • Oka kwa muda wa dakika thelathini.
 • Baada ya keki kupoa, changanya kikombe kimoja cha sukari laini na kijiko kimoja cha maziwa
 • kisha mwaga kwenye keki.
 • Unaweza kuongeza chakuleti iliyoyeuka kwenye keki yako.