Makala

LISHE: Kiamsha kinywa kilicho rahisi kuandaa

June 30th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa matayarisho: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

– uyoga

– mayai 4

– pilipili mboga iliyokatwa nusu

– nyanya 2

– kitunguu maji

– chumvi

– mafuta ya kupikia

– hiliki kijiko ½ cha chai

– masala ya chai kijiko ½ cha chai

– pilipili iliyosagwa

– maziwa vikombe 2

– majani ya chai

– maji vikombe 2

– sukari

Maelekezo

Jinsi ya kupika chai

• weka maziwa, maji kiasi, hiliki, masala ya chai na majani katika sufuria

• chemsha kwa muda wa dakika 10 na chai itakuwa tayari

Jinsi ya kupika mayai

• weka mafuta kiasi katika kikaangio kasha utie vitunguu

• vikaange hadi vitunguu viwe na rangi ya kahawia kasha tia nyanya, chumvi na pilipili mboga

• pika kwa muda wa dakika tano kasha tia mayai na uyaache yaive mpaka yakauke; unatakiwa kugeuza upande wa pili na uyapike mpaka yaive kabla ya kuepua

Mayai. Picha/ Margaret Maina

Jinsi ya kupika uyoga

Uyoga. Picha/ Margaret Maina

• weka mafuta kidogo katika kikaangio kasha tia uyoga na chumvi na ukaange mpaka uive katika moto wa wastani

• ukishaiva, kiamsha kinywa chako kitakuwa tayari

Pakua pamoja na mkate, andazi, viazi vitamu au chochote ukipendacho na ufurahie ukianza siku yako kwa njia ya kipekee.

Chai na slesi ya mkate. Picha/ Margaret Maina