Makala

LISHE NA VINYWAJI: Ni faida zipi mtu anapata kwa kunywa kahawa?

May 29th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KAHAWA ni kinywaji maarufu na kinachopendwa sana na watu wengi.

Kupendwa kwa kinywaji cha kahawa kunatokana na manufaa kadhaa yanayopatikana ndani ya kinywaji hiki.

Huchangamsha mwili

Kahawa huwafanya watu wasijisikie kuchoka na huwaongezea kiwango cha nguvu za mwili. Caffeine inayopatikana kwenye kahawa huuchangamsha ubongo na kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.

Huyeyusha mafuta mwilini

Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kahawa huchangia katika kuyeyusha mafuta mwilini na hivyo kumsaidia mtumiaji wa kinywaji hicho kukabili tatizo la uzani wa juu wa mwili.

Kahawa ina virutubisho muhimu

Kahawa ni kinywaji chenye virutubisho muhimu kwa ajili ya afya za miili yetu.

Hukabili aina ya pili ya kisukari

Kisukari ni ugonjwa ambao mwili hushindwa kudhibiti kiwango cha sukari jinsi inavyostahili. Inakadiriwa kuwa ugonjwa huu unawatesa watu wengi duniani. Watumiaji wa kahawa wana hatari ndogo ya kupata kisukari aina ya pili yaani Type 2 Diabetes.

Huzuia maradhi ya kupoteza kumbukumbu

Maradhi ya kupoteza kumbukumbu huwakabili watu wengi hasa wenye umri wa kuanzia miaka 65

Hulinda afya ya ini

Ini ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu. Hata hivyo maradhi kama vile uvimbe kwenye ini pamoja na tatizo la seli za ini kugeuka makovu huathiri afya ya ini kwa kiasi kikubwa. Kahawa hupunguza uwezo wa seli za ini kuwa makovu kwa asilimia kubwa.

Huondoa msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo ni tatizo baya la kiakili na kisaikolojia ambalo linaweza kuathiri maisha kwa kiasi kikubwa au hata kusababisha kifo.

Inaelezwa kuwa watu wanaokunywa angalau kikombe kimoja cha kahawa kila siku hupunguza msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa.