Makala

LISHE: Namna ya kutengeneza sandwich

June 6th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Walaji: 4

Vinavyohitajika

· Slesi mbili za mkate (kwa kila sandwich)

· Siagi kwa ajili ya kukaangia mkate

· Ham (vipande viwili kwa kila sandwich)

· Cheese

· Nyanya

· Parachichi

Utaratibu

Katakata nyanya na parachichi, weka pembeni.

Paka siagi mkate upande mmoja kila slesi, weka pembeni.

Kwenye kikaango katika moto wa wastani, weka mkate upande wenye siagi kwa chini. Ongeza cheese kwa juu ikifuatiwa na nyanya, parachichi na ham kisha funika na cheese tena juu.

Ongeza slesi ya mkate; upande uliopakwa siagi juu.

Kaanga pande zote za mkate mpaka uwe wa kahawia kiasi na cheese iyeyuke.

Pakua na ufurahie wakati unakunywa chai au juisi.