Habari Mseto

Lita 4,500 za Dizeli ya soko la nje zanaswa Kisumu

August 24th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

TUME ya Kudhibiti Mafuta nchini (ERC) Ijumaa imetoa taarifa kuhusu operesheni kumaliza biashara haramu ya mafuta eneo la Otonglo, Kaunti ya Kisumu.

Operesheni hiyo ilifanywa Jumatano na maafisa wa uchunguzi wa kihalifu (DCI) na police wa  GSU ambao walipata lita 4,500 za dizeli ya kuuza nje.

Wakati wa operesheni hiyo, washukiwa watano walikamatwa na gari lenye nambari ya usajili KAN 022 C. Watano hao walifikishwa mahakamani Jumatano na kushtakiwa kwa kuendesha biashara bila leseni kinyume cha sheria.

Kituo hicho pia kiliharibiwa kwa mujibu wa sheria, ilisema ERC.