Liverpool na Salah wavutania mshahara

Liverpool na Salah wavutania mshahara

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL watakuwa radhi kuachilia mfumaji Mohamed Salah kuyoyomea Real iwapo wafalme hao wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) na Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) wataweka mezani Sh8.8 bilioni.

Kuondoka kwa Salah, 30, huenda kukavujisha zaidi safu ya mbele ya Liverpool ambao tayari wameagana na Sadio Mane aliyejiunga na Bayern Munich ya Ujerumani kwa Sh5 bilioni.

Salah ambaye amesalia na mwaka mmoja pekee katika mkataba wake wa sasa na Liverpool, anadai mshahara wa Sh59 milioni kwa wiki ili arefushe muda wa kuhudumu kwake ugani Anfield.

Ingawa Liverpool wana hamu ya kudumisha Salah kambini mwao, hawako radhi kuzidisha gharama yao ya matumizi ya fedha ili kuridhisha matamanio ya nyota huyo raia wa Misri.

Ujira wa Sh30 milioni kwa wiki unafanya Salah kwa sasa kuwa sogora wa pili nyuma ya beki Virgil van Dijk (Sh32.6 milioni) anayedumishwa kwa mshahara wa juu zaidi ugani Anfield.

Kuhama kwa Salah kutasaza Liverpool katika ulazima wa kutegemea zaidi maarifa ya Roberto Firmino, Diogo Jota, Luis Diaz na Darwin Nunez katika safu yao ya mbele. Kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp kimeagana pia na wavamizi Divock Origi na Takumi Minamino.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Hii ya Ronaldo kuenda Chelsea ni hatari!

Kocha Wayne Rooney ataka vinara wa Derby County wamwachishe...

T L