Liverpool nguvu sawa na Crystal Palace katika EPL baada ya Nunez kuonyeshwa kadi nyekundu

Liverpool nguvu sawa na Crystal Palace katika EPL baada ya Nunez kuonyeshwa kadi nyekundu

Na MASHIRIKA

FOWADI Luis Diaz alisaidia waajiri wake Liverpool kujizolea alama moja baada ya kulazimishia Crystal Palace sare ya 1-1 katika pambano la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumatatu usiku ugani Anfield.

Liverpool ya kocha Jurgen Klopp ilikamilisha mchuano huo na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya mvamizi mpya Darwin Nunez kuonyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili.

Licha ya Liverpool kutamalaki mchezo katika kipindi cha kwanza, Palace waliwekwa kifua mbele na Wilfried Zaha aliyeshirikiana vilivyo na kiungo mvamizi, Eberechi Eze.

Nunez alionyeshwa kadi nyekundu na refa Paul Tierney baada ya kumpiga beki Joachim Andersen wa Palace kwa kichwa. Japo tukio hilo la kupunguzwa wa wachezaji wa Liverpool liliwapa Palace motisha zaidi, Diaz alisawazisha mambo kunako dakika ya 61 baada ya kumwacha hoi kipa Vicente Guaita.

Sawa na Mo Salah na Fabio Carvalho wa Liverpool, Palace nao walipoteza nafasi nzuri za wazi kupitia Zaha. Liverpool waliokamilisha kampeni za EPL msimu jana katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City, sasa wanakamata nafasi ya 12 kwa alama mbili, moja zaidi kuliko Palace wanaokamata nafasi ya 16. Liverpool walifungua kampeni zao za EPL msimu huu kwa sare ya 2-2 dhidi ya Fulham huku Palace wakipepetwa 2-0 na Arsenal uwanjani Selhurst Park.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

IEBC yachapisha rasmi kwa gazeti la serikali Ruto ndiye...

SHINA LA UHAI: Je, ni ushirikina, laana au ugonjwa?

T L