Liverpool wamsajili kinda matata wa Fabio Carvalho kutoka Fulham

Liverpool wamsajili kinda matata wa Fabio Carvalho kutoka Fulham

NA MASHIRIKA

LIVERPOOL wamemsajili fowadi chipukizi Fabio Carvalho kutoka Fulham kwa mkataba wa miaka mitano uliogharimu Sh1.2 bilioni.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, atatua rasmi ugani Anfield mnamo Julai 1, 2022. Ushawishi wa chipukizi huyo ulichangia pakubwa kupandishwa kawao hadi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu baada ya kupachika wavuni mabao 10 na kuchangia mengine manane.

Liverpool nusura wamsajili Carvalho mnamo Januari 2022 ila mpango huo ukakosa kuzaa matunda.

Carvalho aliyepokezwa malezi ya soka katika akademia ya Fulham, alichezea kikosi cha makinda wa Uingereza kabla ya kubadilisha uraia na kuanza kusakatia kikosi cha Ureno cha U-21 mnamo Machi 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Uhuru awataka wawaniaji wakubali matokeo ya uchaguzi wa...

Tetesi: Arsenal, Dortmund wamezea mate beki Okumu

T L