Michezo

Liverpool yatoa nyota wengi kwenye kikosi cha bara Uropa

June 4th, 2019 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

MABINGWA wapya wa soka ya Klabu Bingwa Ulaya, Liverpool wametambulia kwa juhudi zao katika makala ya mwaka huu kwa wachezaji wake sita kutajwa katika kikosi cha wachezaji 20 waliong’ara katika msimu 2018-2019.

Vijana wa kocha Jurgen Klopp, ambao walichabanga Tottenham Hotspur 2-0 katika fainali jijini Madrid nchini Uhispania hapo Juni 1, wanajivunia kuwa na wachezaji Alisson Becker, Virgil van Dijk ambaye aliibuka mchezaji bora katika fainali, Trent Alexander-Arnold, Andy Robertson, Georginio Wijnaldum na Sadio Mane katika kikosi hicho kinachoundwa na wataalamu wa kiufundi kutoka Shirkisho la Soka barani Ulaya (UEFA).

Uamuzi wa wataalamu hao unazingatia mchango uliotolewa na wachezaji hao katika klabu zao msimu huu.

Mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2017 na 2018, Mohamed Salah hakupata namba. Wachana-nyavu matata Cristiano Ronaldo (Juventus) na Lionel Messi, ambao ni washindi mara tano wa tuzo ya kifahari ya Ballon d’Or, wamo katika kikosi hiki ambacho pia kimeshuhudia Tanguy Ndombele kutoka Lyon nchini Ufaransa akipata namba.

Hii hapa orodha yote ya wachezaji 20 waliong’aa msimu 2018-2019 kiasi ya kuvutia macho ya wataalamu na kutambuliwa kwa juhudi zao.

Liverpool

Alisson Becker (Kipa, Brazil)

Virgil van Dijk (Beki, Uholanzi)

Trent Alexander-Arnold (Beki, Uingereza)

Andrew Robertson (Beki, Scotland)

Georginio Wijnaldum (Kiungo, Uholanzi)

Sadio Mane (Mshambuliaji, Senegal)

Ajax Amsterdam

David Neres (Mshambuliaji, Brazil)

Dusan Tadic (Kiungo, Croatia)

Frenkie De Jong (Kiungo, Uholanzi)

Hakim Ziyech (Kiungo, Morocco)

Matthijs De Ligt (Beki, Uholanzi)

Tottenham

Jan Vertonghen (Beki, Ubelgiji)

Moussa Sissoko (Kiungo, Ufaransa)

Lucas Moura (Kiungo, Brazil)

Barcelona

Marc-Andre ter Stegen (Kipa, Ujerumani)

Lionel Messi (Mshambuliaji, Argentina)

Juventus

Cristiano Ronaldo (Mshambuliaji, Ureno)

Manchester City

Raheem Sterling (Mshambuliaji, Uingereza)

Kevin De Bruyne (Kiungo, Ubelgiji)

Lyon

Tanguy Ndombele (Kiungo, Ufaransa)