Dondoo

Lofa atatizwa na mke kutaja jina la jirani wakiburudishana

June 12th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

NYALI, MOMBASA

JOMBI wa hapa amechanganyikiwa baada ya mkewe kutaja jina la jirani yao akipiga nduru kwa raha wakichangamshana chumbani.

Jamaa aliambia mabeshte wake wakiwa baa kwamba anashuku mkewe huwa anachepuka na jamaa huyo na anafurahia ngoma akiwa naye.

“Haiwezi kuwa bure apige nduru akitaja jina la mwanamume tena jirani. Inaonekana wamekuwa wakirushana roho na hii imenitia wasiwasi sana,” jamaa alisema na kuongeza kuwa mkewe alikataa kutoka na mwanamume huyo.

Hata hivyo, wenzake walimwambia asimwamini ila afanye uchunguzi na atabaini ukweli.

Jamaa alisema tangu kisa hicho, hamchangamkii mkewe kamwe.