Michezo

Lukaku, Lingard, Sanchez, Bailly na Martial wananimezea mate, nifanyaje?

July 14th, 2019 2 min read

Na CHRIS ADUNGO

WIKI chache baada ya Fanny Neguesha kumtaka mwanasoka Mario Balotelli kumkoma kabisa, mwanamitindo huyo wa Ubelgiji amefichua kwamba ndoa kati yake na kiungo Mario Lemina wa Southampton inayumbishwa na mawimbi mapya.

Hii ni baada ya kichuna huyo mwenye umri wa miaka 29 kukiri kunyemelewa mitandaoni na majanadume ya Manchester United ambayo kwa mtazamo wake, yana nia ya kumvurugia ndoa.

Kulingana naye; Romelu Lukaku, Jesse Lingard, Alexis Sanchez, Eric Bailly na Anthony Martial wamekuwa wakilihemea pakubwa penzi lake kwa kurusha picha na jumbe za kumtia kishawishini aachane na Lemina tangu mumewe huyo aanze kuhusishwa na uwezekano wa kuhamia uwanjani Old Trafford muhula huu.

Katika mahojiano yake na gazeti la The Sun, Neguesha aliungama kwamba wengi wa wanaume wanaomvizia ni wachezaji na mashabiki wa Man-Utd ambao walimfahamu wakati alipokuwa akitoka kimapenzi na Balotelli aliyekuwa sogora wa Man-City.

Madai ya Neguesha yanajiri mwezi mmoja baada ya kuungama kwamba Balotelli amekuwa akiwania fursa ya kuanza kulitikisa upya buyu lake la asali.

“Ana namba nyingi za simu. Mara anatuma ujumbe, mara anapiga simu, mara anarusha picha. Nahofia hili litaanza kumkera Lemina ambaye amenivumilia sana,” akasema kwa kusisitiza kwamba sasa haoni sababu yoyote ya mumewe kutua Old Trafford iwapo hali itakuwa hivyo jijini Manchester.

Maamuzi ya Balotelli kuliwania tena tunda la Neguesha yalichochewa na hatua ya kichuna huyo kuusifia utenda-kazi wa nyota huyo kila walipokuwa wakishiriki miereka ya faraghani hapo awali.

Katika mojawapo ya kauli zake, alisema bado hajampata fundi wa mahaba anayemzidi Balotelli kwa ujuzi wa kukitalii kisima chake cha maji makuu. Kulingana naye, wepesi wa jembe la Lemina ni kiini cha kutolimika ipasavyo kwa shamba alilojaliwa nalo, na ambalo hapo awali, lilielekea kuzoea kulimwa kwa mitambo mizito isiyozimika upesi.

“Balotelli si dume linalotisha uwanjani pekee. Pia ni gwiji wa mechi za chumbani. Sijaona kati ya wote waliowahi kumenya tunda hili, anayeweza kukifikia kiwango cha fowadi huyo. Ingawa hivyo, kwa sasa nimepania kutulia katika ndoa ili nimzalie Lemina watoto zaidi,” akasema.

Kwa pamoja na Lemina, videge hao wamejaliwa mtoto wa kiume: Isiah-King. Neguesha ambaye ana historia ya kuwa mwepesi wa kujilegeza kimapenzi kwa wanasoka maarufu wenye vipochi vinono kihela, sasa anamtaka mumewe ajiunge na Arsenal.

Neguesha alitemana na Balotelli mnamo 2014 baada ya kuhusiana kwa miezi 18. Mbali na Balotelli, Neguesha amewahi pia kutoka kimapenzi na kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Senegal, Cheikhou Kouyate, 29, na mwanamuziki mzawa wa Canada, Aubrey Drake, 32.