Lukaku na Young watozwa faini kwa kukiuka kanuni za corona nchini Italia

Lukaku na Young watozwa faini kwa kukiuka kanuni za corona nchini Italia

Na MASHIRIKA

ROMELU Lukaku na Ashley Young ni miongoni mwa wanasoka wanne wa Inter Milan ambao wamepigwa faini ya Sh1.5 milioni kwa kukiuka baadhi ya kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini Italia.

Lukaku, Young, Ivan Perisic na Achraf Hakimi walikuwa katika kundi la watu 23 walioonekana wakila pamoja katika hoteli baada ya kusajili ushindi wa 3-1 dhidi ya AS Roma katika mchuano wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo Mei 12, 2021 usiku.

Ilivyo, miongoni mwa kanuni za kudhibiti janga la corona nchini Italia ni kudumishwa kwa kafyu ya kutopatikana nje kati ya saa nne usiku na saa kumi na moja alfajiri.

Inter walitawazwa mabingwa wa Serie A mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11 na hivyo kukomesha ukiritimba wa Juventus waliokuwa wakiwania taji hilo kwa msimu wa 10 mfululizo.

Mnamo Aprili 2021, wanasoka watatu wa Juventus – Weston McKennie, Paulo Dybala na Arthur Mello pia walitozwa faini ya Sh1.5 kila mmoja kwa kuvunja masharti ya corona.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

 

  • Tags

You can share this post!

UEFA: Fainali ya Man City na Chelsea kuandaliwa jijini...

Sichukii wanaume, ninazingatia haki ninapotoa uamuzi...