Habari Mseto

Maafisa wa usalama wapigwa risasi na majambazi Meru

November 14th, 2020 1 min read

DAVID MUCHUI NA FAUSTIN NGILA

Maafisa wanane wa polisi pamoja na mkazi mmoja walipata majeraha bada ya kupigwa risasi na wavamizi waliovamia eneo la Makinya Igembe Kaskazini Kaunti ya Meru Ijumaa jioni.

Tukio hilo lilijiri siku moja baada ya wavamizi kutoka Kuanti jirani ya Isiolo kuvamia wafungaji na kuumiza wawili Alhamisi.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Meru John Mwanzia  alisema kwamba walioumia ni afisa wa GSU na watano wa  ASTU Pamoja na mwendesha bodaboda.

Bw Mwanzia alisema kwamba maafisa hao wa polisi walivamiwa walipokuwa wakifanya patrol kwenye eneo la malisho ambapommauaji hayo yalitokea Alhamisi.

 

Wafungaji kutoka Meru na Turkana wamekuwa kizozania eneo la kilomita 6340 ambayo inatumika kama eneo la malisho kwa wafungaji wa Meru na kitambo ilikuwa hifadhi ya Nyambene..
“Maafisa hao walipata majeraha miguuni na mikononi na wako sawa.Maafisa watatu wako kwenye hospitali ya Maua Methodist huku wengine watano wa GSTU wako kwenye hospitali ya rufaa yay a Isiolo,”alisema Bw Mwanzia.

Kamanda wa polisi alisema kwamba mzozo ambao umekuwa juu ya eneo hilo la malisho unapaswa kuangaziwa na wanasiasa.

“Polisi hawawezi kusuisha mzozo wa ardhi.Tuanataka  wizara ya ardhi ,viogozipamoja na jamii wakuje Pamoja kusuisha mzozo huo,”alisema.