Habari Mseto

Maafisa wa zamani wa kaunti watozwa faini

September 5th, 2020 1 min read

Na Rushdie Oudia

Korti ya Kisumu imewatoza faini  maafisa watatu wa zamani wa Kaunti ya Siaya Sh1 milioni walipopatikana na hatia ya kukiuka mikakati ya ununuzi katika kutolewa kwa zabuni ya kununua bidhaa za michezo iliyogharimu Sh14.9 milioni.

Watatu hao ni aliyekuwa naibu kamishena wa kaunti Kepher Marube, aliyekuwa mkuu wa ununuzi Zakayo Ojuok na mkurugenzi wa usambazaji bidhaa, Tobias Odongo Oloo.

Hakimu Robinson Ondieki alisema kwamba Marube na Odongo watafungwa kwa muda wa mwaka moja wakishindwa kulipa thamana hio huku Ojuok akifungwa miaka mitatu.

Watatu hao walipatikana na hatia mingi ikiwemo udanganyifu,utumizi mbaya wa afisi na  kukosa  kuzingatia sheria.

Wanasheria wanaowakilisha  watatu hao wanajaribu kuiomba korti iwape watatu hao dhamana ya haki au kifungo cha nje.

Tafsiri Na Faustine Ngila