Habari za Kitaifa

Maafisa watano wa DCI wanaswa TZ wakichunguza wizi wa magari

May 24th, 2024 1 min read

ANTHONY KITIMO Na STANLY NGOTHO

MAAFISA watano wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kutoka kituo cha polisi cha Buruburu, Nairobi walizuiliwa nchini Tanzania kwa saa sita baada ya kukamatwa wakifuatilia kisa cha wizi wa magari.

Maafisa hao walitiwa mbaroni Ijumaa eneo la Tarakea walipomkamata mshukiwa kwa madai ya kuiba gari na kutorokea nchini humo.

Kulingana na ripoti ya polisi, maafisi hao walisemekana kuingia Tanzania bila kujitambulisha na hivyo basi kutiwa mbaroni.

Tayari maafisa hao wamepelekwa katika kituo cha polisi cha makao makuu ya Rombo ambapo wanazuiliwa.

Maafisa hao Ali Ibrahim, Joel Osinya, Moses Wainaina, Josephat Munginia na Moses Kiongea wote kutoka Nairobi ndio walizuiliwa na wenzao wa Tanzania.

Baada ya majadiliano ya awali kugonga mwamba, walihamishiwa kituo cha Rombo.

Hata hivyo waliachiliwa baada ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni kuingilia kati.